CALIFORNIA, MAREKANI

Jeshi la Anga la Marekani limepata pigo kubwa baada ya moja ya ndege zake muhimu na zenye nguvu zaidi, aina ya B-52 Stratofortress, kuanguka muda mfupi baada ya kupaa katika jimbo la California.

Ndege hiyo, ambayo inachukuliwa kuwa uti wa mgongo wa mashambulizi ya masafa marefu ya Marekani, inaripotiwa kuwa miongoni mwa zana zilizokuwa zikishiriki katika operesheni za kijeshi nchini Iran wakati huu wa mivutano ya kivita kati ya Marekani, Israel, na Iran.

Uwezo wa Kutisha wa B-52

Ndege ya B-52 ni kielelezo cha nguvu ya kijeshi ya Marekani. Ina uwezo wa kupaa hadi kimo cha futi 50,000—juu zaidi ya ndege za abiria ambazo hupaa kimo cha futi 35,000. Aidha, ndege hii ina uwezo wa kubeba shehena ya silaha yenye uzito wa ratili (lbs) 70,000, ikijumuisha mamia ya mabomu ya kawaida na makombora 32 ya nyuklia (nuclear cruise missiles).

Sifa ya kipekee ya B-52 ni uwezo wake wa kuongezewa mafuta ikiwa angani, jambo linaloifanya kuwa na uwezo wa kushambulia mahali popote duniani bila kuhitaji kutua. Wakati wa enzi za Vita Baridi, ndege hii ilitumika kama “mwavuli wa nyuklia” wa Marekani chini ya sera ya maangamizi ya pande zote (Mutually Assured Destruction)

Leave a Reply