Rais Donald Trump anatarajiwa kufanya mkutano katika Chumba cha kusimamia migogoro (Situation Room) jijini White House siku ya Jumatatu kuhusu suala la Iran, pamoja na timu yake ya juu ya usalama wa taifa na sera za kigeni.Kwa mujibu wa ripoti ya Axios, mkutano huo umethibitishwa na maafisa watatu wa Marekani.Chanzo kimoja kilisema kuwa timu ya Trump itajadili mkwamo uliopo katika mazungumzo na hatua zinazoweza kuchukuliwa baadaye.Mgogoro katika mazungumzo kati ya Marekani na Iran ulizidi mwishoni mwa wiki baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, nchini Pakistan kumalizika bila maendeleo yoyote.Ziara hiyo ilikuwa moja ya juhudi za kufufua mazungumzo yanayohusu kusitisha mapigano na kufikia makubaliano ya kudumu, lakini haikuleta matokeo yanayoonekana.Habari hii inakuja wakati mvutano kati ya Washington na Tehran unaendelea, huku upande wa Marekani ukisisitiza kuwa ina “kadi zote” mkononi mwake, na upande wa Iran ukisisitiza masharti yake kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja.