Gazeti moja nchini Marekani limeripoti kuwa utafiti mpya wa Taasisi ya Manhattan umeonesha matokeo ya kushangaza kuhusu mtazamo wa wanachama wa chama cha Democratic kufuatia jaribio la kumuua rais, Donald Trump.
Kwa mujibu wa utafiti huo, takribani asilimia 47 ya Wanademokrasia wanaamini kuwa jaribio la kumuua Trump lililotokea mjini Butler, jimbo la Pennsylvania, wakati wa kampeni zake za uchaguzi, lilipangwa na kuandaliwa na wafuasi wake wenyewe ili kuongeza uungwaji mkono kwake kisiasa.
Ripoti hiyo imezua mjadala mpana katika medani za kisiasa Marekani, huku wachambuzi wakitaja matokeo hayo kuwa ishara ya kuongezeka kwa kutokuaminiana kati ya wafuasi wa vyama vikuu nchini humo.
w