Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa matamshi mapya kuhusu Iran, akisisitiza msimamo mkali juu ya suala la nyuklia pamoja na maendeleo ya hali ya kiusalama katika eneo la Ghuba.Trump amesema kuwa “Marekani haiwezi kuruhusu Iran kupata silaha za nyuklia kwa njia yoyote ile.” Ameeleza kuwa hatua hiyo, kwa mtazamo wake, itahatarisha usalama wa kimataifa.a
Aidha, katika kauli zake, alidai kuwa kuna kiasi kikubwa cha mafuta kilichopo katika Mlango wa Hormuz na kwamba yakiachiliwa sokoni, bei ya petroli inaweza kushuka kwa kiwango ambacho hajawahi kushuhudiwa.
Akitaja uvamizi wa sasa wa Marekani dhidi ya Iran, Trump alisema kuwa Marekani “inaongoza na kushinda katika mgogoro huo,” akifananisha hali hiyo na pambano ambalo, kwa maelezo yake, “lingesimamishwa mara moja kutokana na kutokuwa na uwiano.”