Mwamuzi nyota kutoka Somalia, Omar Artan, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini Marekani, hali ambayo imezua maswali mengi kuhusu hatma yake ya kuchezesha katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2026.

Artan, ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya FIFA tangu mwaka 2018 na ambaye hivi karibuni alitunukiwa tuzo ya Mwamuzi Bora wa Mwaka wa Wanaume wa CAF kwa mwaka 2025, alikuwa amejumuishwa kwenye orodha ya maofisa 52 waliochaguliwa kusimamia michuano hiyo mikubwa duniani.

Kufikia sasa, sababu za kuzuiliwa kwake kuingia nchini humo hazijawekwa wazi, huku wadau wa soka wakisubiri kuona hatua zitakazochukuliwa na mamlaka husika, ikiwemo FIFA, kufuatia tukio hili linaloweza kumtoa mwamuzi huyo kwenye kinyang’anyiro cha kuchezesha katika michuano hiyo ya kihistoria.

Tutazidi kuwapa taarifa zaidi kadiri tutakavyozidi kupata undani wa kisa hiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *