Mbunge wa Republican Thomas Massie ametoa madai kwamba rais wa Marekani Donald Trump alitumia mamlaka yake ya veto kama hatua ya kisiasa dhidi ya mbunge Lauren Boebert, kufuatia msimamo wake kuhusu nyaraka za siri zinazohusiana na Jeffrey Epstein.
Kwa mujibu wa Massie, Boebert aliitwa katika chumba maalum cha dharura cha Ikulu ya Marekani, kinachotumika kwa operesheni nyeti za kijeshi, ambapo aliwekwa chini ya shinikizo kubwa kuondoa jina lake kwenye ombi la kutaka nyaraka za Epstein ziwekwe wazi kwa umma.
Massie amesema kuwa baada ya Boebert kukataa kubadilisha msimamo wake, Trump alipinga kupitia veto mswada uliokuwa umeidhinishwa kwa kauli moja, uliolenga kupeleka huduma ya maji katika maeneo makubwa ya kusini mwa jimbo la Colorado.
Aidha, Massie amedai kuwa hatua hiyo haikutokana na sababu za kiufundi wala kiuchumi, bali ilikuwa ni “kisasi cha kisiasa”. Kwa mujibu wa madai hayo, takriban watu 50,000 wameathiriwa kwa kukosa huduma ya maji safi kutokana na uamuzi huo.Hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa mara moja kuhusu madai hayo.