Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amejikuta katika wimbi zito la ukosoaji kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kauli yake ya kulaani matumizi ya nguvu, muda mfupi baada ya jaribio la kumuua Rais wa Marekani, Donald Trump. Katika taarifa yake, Netanyahu alisema wazi kuwa, “Hakuna nafasi ya ghasia; si dhidi ya viongozi wa kisiasa, wala dhidi ya mtu mwingine yeyote.” Hata hivyo, kauli hiyo imepokelewa kwa hisia mseto, huku makala moja ikimwelezea kwa maneno makali na kumuita “Gaidi analiyeua watoto wengi zaidi duniani.” Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wametumia fursa hiyo kukosoa na kudhihaki matamshi hayo, wakikumbusha operesheni za jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza na tuhuma za mauaji ya viongozi mbalimbali wa Iran, Palestina, na Lebanon.