Jean-Luc Mélenchon, mgombea wa urais wa Ufaransa, amesema kuwa Israel kwa sasa ndiyo nchi hatari zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Ameieleza Israel kuwa ndiyo inayowashambulia majirani zake, kuchochea vita, na kutekeleza mauaji ya kimbari, akibainisha kuwa anapoitaja Israel analenga serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Katika kauli nyingine, Mélenchon amesema aliwahi kumuuliza jenerali anayesimamia kikosi cha Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ambazo zingechukuliwa iwapo Netanyahu angeivamia Lebanon. Kwa mujibu wa Mélenchon, jenerali huyo alimjibu kuwa maagizo yao ni kujiondoa.
Mélenchon amesema hakuelewa namna kikosi cha kulinda amani kinaweza kujiondoa badala ya kuingilia kati ili kuzuia mapigano.Aidha, amesema kuwa iwapo askari wa Ufaransa atashambuliwa, basi Ufaransa inapaswa kujibu.
Pia amesisitiza kuwa ndege za Marekani hazipaswi kuruka juu ya anga ya Ufaransa wala kutumia kambi za kijeshi za Ufaransa, akieleza wazi kuwa anapinga hali hiyo.