Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amewafukuza kazi Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Fedha. Waziri wa Fedha alikuwa amehudumu katika wadhifa huo chini ya wiki mbili.

Hatua hiyo ni mabadiliko ya hivi karibuni katika safu ya juu ya serikali ya Kiir inayoyumbayumba.

Mkuu wa jeshi la Sudan Kusini aliyefutwa kazi, Jenerali Paul Nang, alishika wadhifa huo Oktoba mwaka jana na tangu wakati huo alikuwa akichunguzwa kufuatia hali mbaya ya ukosefu wa usalama nchini humo.

Waziri wa Fedha, Salvatore Garang Mabiordit ambaye pia amefukuzwa kazi na Rais Kiir, amehudumu katika nafasi hiyo tangu Aprili 23 mwaka huu, yaani muda wa chini ya wiki mbili.

Baada ya kuwafuta kazi Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Fedha, Rais wa Sudan Kusini amemteuwa tena Jenerali Santino Deng Wol kuwa Mkuu Jeshi.

Wol, ambaye anatoka katika eneo la Bahr El Gazal nchini Sudan Kusini ambako Kiir anatoka, ni mshirika wake wa karibu na aliwahi kuhudumu katika wadhifa huo kati ya mwaka 2020 na 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *