Beijing — Katika hatua ya kushangaza huku kukiendelea msako ndani ya jeshi lake, China siku ya Alhamisi iliwapa mawaziri wake wawili wa zamani wa ulinzi adhabu ya kifo iliyoahirishwa kwa tuhuma za ufisadi.
Wei Fenghe na Li Shangfu wote walipatikana na hatia ya kupokea rushwa na wakahukumiwa adhabu ya kifo yenye kusitishwa kwa miaka miwili na mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
Mahakama ilitangaza kuwa baada ya miaka miwili, adhabu zao zitabadilishwa kuwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kupewa msamaha.Wei, mwenye umri wa miaka 72, alihudumu kama waziri wa ulinzi kuanzia 2018 hadi 2023. Li, mwenye umri wa miaka 68, alichukua nafasi ya Wei na kushikilia wadhifa huo kwa chini ya miezi minane mwaka 2023.
Wote wawili waliwekwa chini ya uchunguzi na kitengo cha kupambana na ufisadi cha jeshi mwaka 2023.