Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ameonya kuwa uwezekano wa kuondoa vikwazo dhidi ya Iran haupo kabisa hadi pale Mlango wa Hormuz utakapofunguliwa, akibainisha msimamo mkali wa Paris kuhusu hali inayoendelea katika eneo la Asia ya Magharibi.
Akizungumza leo kwenye mahojiano maalum na kituo cha redio na televisheni cha RTL, waziri huyo aliweka wazi misimamo miwili mikuu: Kwanza, kusisitiza kuwa hatua yoyote ya kuondoa vikwazo haitazingatiwa wakati njia muhimu ya kimkakati kama Hormuz ipo katika hali ya kuzuiwa.
wPili, aliitaka Ulaya kuelekeza nguvu zaidi katika kupunguza utegemezi ambao, kwa maneno yake, “umeilazimisha kulipia gharama za vita ambavyo si chaguo lake.”Katika mahojiano hayo yaliyofanyika saa chache kabla ya kutolewa kwa jibu la Iran kuhusu pendekezo la amani la Marekani, waziri alisema Iran—inayodai kuhitaji kuondolewa kwa vikwazo kama sehemu ya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia—haiwezi kutarajia hatua hiyo huku hali ya usalama katika Mlango wa Hormuz ikiwa bado tete.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *