Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kumkosoa vikali Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, katika chapisho lake la Truth social akisema kwamba anapaswa kuelekeza juhudi zaidi katika jitihada za kukomesha vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, ambavyo amedai kwamba hadi sasa havijaonyesha mafanikio makubwa chini ya uongozi wake.
Ameongeza kuwa kiongozi huyo pia anapaswa kushughulikia changamoto zinazokabili taifa lake, ikiwemo masuala ya uhamiaji na nishati, badala ya kujihusisha na mambo yanayohusu mataifa yanayopambana kutokomeza tishio la nyuklia la Iran.Kwa mujibu wa Rais wa Marekani, Donald J. Trump, hatua hizo zingesaidia kuifanya dunia, ikiwemo Ujerumani, kuwa mahali salama zaidi.