Rais wa Meksiko, Claudia Sheinbaum, ametangaza rasmi kuwa nchi yake itaikaribisha timu ya taifa ya soka ya Iran katika mji wa Tijuana kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia.

Uamuzi huo wa upendo umekuja baada ya Marekani kukataa kutoa kibali kwa timu hiyo ya Iran kuweka kambi na kukaa katika jimbo la Arizona.

Hatua hiyo ya Marekani ilizua sintofahamu kuhusu mahali ambapo timu hiyo ingefanyia maandalizi yake, kabla ya Rais Sheinbaum kuingilia kati na kutoa mji wa Tijuana kama mbadala.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Sheinbaum amethibitisha kuwa Meksiko iko tayari kutoa ushirikiano kamili kwa wanamichezo hao ili kuhakikisha wanaendelea na ratiba yao bila hitilafu yoyote.

Suala hili limevuta hisia za wengi katika ulimwengu wa soka, huku Tijuana ikitarajiwa kuwa kitovu cha maandalizi ya Iran kuelekea kilele cha michuano hiyo mikubwa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *