Mgombea wa urais wa Ufaransa Jean‑Luc Mélenchon amesema kuwa migogoro ya sasa ya kimataifa inaweza kuashiria mwisho wa kile alichokiita “karne ya Marekani”.
wAkizungumzia nafasi ya Marekani katika mfumo wa kimataifa, Mélenchon alisema kuwa nguvu ya Marekani haitokani sana na uwezo wake wa kijeshi bali na nafasi ya dola ya Marekani katika uchumi wa dunia. Kwa mujibu wake, dola ndiyo msingi mkuu wa ushawishi wa Marekani.
Aliongeza kuwa Marekani imejizatiti kijeshi ili kuhakikisha kuwa dola inaendelea kuwa sarafu yenye nguvu katika biashara ya kimataifa. Hata hivyo, alisema kuwa polepole baadhi ya benki kuu duniani zinaanza kupunguza utegemezi wao kwa sarafu hiyo.