Poland siku ya Alhamisi imeandika historia kwa kusajili rasmi ndoa yake ya kwanza ya watu wa jinsia moja, kufuatia maamuzi ya mahakama za Poland na Umoja wa Ulaya yaliyoagiza kutambuliwa kwa ndoa za aina hiyo zilizofungwa nje ya nchi.
Meya wa jiji la Warsaw, RafaĆ Trzaskowski, amesema kuwa mamlaka ya jiji hilo tayari imetoa usajili wa kwanza wa cheti cha ndoa kwa wanandoa wa jinsia moja kwa kuzingatia maamuzi ya mahakama.
Aidha, Trzaskowski amesema Warsaw itaanza kutambua moja kwa moja ndoa nyingine za watu wa jinsia moja zilizosajiliwa katika mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya, hata kama hakutakuwa na uamuzi maalum wa mahakama kwa kila kesi.