Watangazaji wa umma nchini Ireland na Hispania wametangaza kususia shindano la mwaka huu la Eurovision Song Contest wakipinga ushiriki wa Israel.Shirika la utangazaji la Hispania, RTVE, limethibitisha kuwa halitarusha matangazo ya shindano hilo, huku RTÉ ya Ireland ikisema haitatangaza wala kushiriki kabisa katika tukio hilo. RTÉ imeeleza uamuzi huo kuwa ni kwa sababu ushiriki wa Israel “haukubaliki kabisa” wakati mgogoro wa kibinadamu ukiendelea katika Ukanda wa Gaza.Hatua hiyo imekuja wakati shinikizo linaendelea kuongezeka dhidi ya waandaaji wa Eurovision kuhusu kujumuishwa kwa Israel, huku maelfu ya wasanii duniani wakitoa wito wa kususia na kuitaka Israel ipigwe marufuku kushiriki katika mashindano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *