Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametangaza mwanzo wa “sura mpya” kwa Mlango Bahari wa Hormuz, njia ya kimkakati ya baharini.
Aidha amesisitiza kuwa Iran itaweka kanuni mpya za usimamizi katika Mlango wa Bahari wa Hormuz kufuatia uchokozi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel dhidi ya nchi hiyo.
Ayatullah Khamenei alitoa kauli hizo katika ujumbe uliotolewa Alhamisi kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Ghuba ya Uajemi. Kila mwaka tarehe 30 Aprili, Iran hukumbuka ushindi wake wa kihistoria wa mwaka 1622 dhidi ya utawala wa kikoloni uliokuwa umeikalia kwa mabavu sehemu ya pwani yake ya kusini.
Maadhimisho ya mwaka huu yamekuja hasa miezi miwili tangu Marekani na utawala wa Israel walipoanzisha vita vya kichokozi dhidi ya Iran tarehe 28 Februari.
Katika ujumbe wake, Ayatullah Khamenei ameitaja Ghuba ya Uajemi kuwa ni “neema isiyoweza kubadilishwa” kwa mataifa ya Kiislamu ya eneo hilo.