KYIV, UKRAINE – Mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, upo katika hali ya taharuki kufuatia majeshi ya Urusi kuanzisha wimbi jipya la mashambulizi ya kimkakati yanayolenga viwanda na asasi mbalimbali za kijeshiKutokana na operesheni hiyo, Serikali ya Urusi imetoa onyo kali na kuwashauri raia wote wa kigeni kuondoka haraka iwezekanavyo mjini humo. Wakati huo huo, wakazi wa Kyiv wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa kwa kutokusogelea maeneo yote ya miundombinu ya kijeshi na ofisi za kiutawala ili kunusuru maisha yaKwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Urusi, uamuzi wa kuzidisha mashambulizi haya unakuja kama majibu ya shambulio la Starobilsk, tukio ambalo Urusi imeeleza kuwa limefikisha mwisho ukomo wa uvumilivu waoKatika awamu hii, mashambulizi ya Urusi yameelekezwa rasmi kwenye maeneo yanayotumika kusanifu, kuzalisha, na kuandaa matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) za Ukraine. Aidha, operesheni hiyo inalenga moja kwa moja vituo vya kufanyia maamuzi na ofisi kuu za makamanda wa kijeshiHatua hii inaashiria mwelekeo mpya na hatari zaidi katika mgogoro huu, huku kukiwa na hofu ya kuwepo kwa mpango mkakati wa kuiharibu kabisa Kyiv. Kinadharia, inakadiriwa kuwa huenda ikachukua muda wa mwezi mmoja pekee kuufanya mji huo mkuu usiweze tena kukalika na binadamu Kwa sasa, macho na masikio ya ulimwengu yanaelekezwa nchini humo kusubiri na kuona iwapo matamshi haya mazito ya kidiplomasia na kijeshi yataakisiwa na vitendo halisi katika uwanja wa vita.#utaridi