🔹 Kituo cha 12 cha Israel, kikinukuu ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, kilithibitisha kuwa Benjamin Netanyahu alifanya ziara ya siri nchini Umoja wa Falme za Kiarabu katika kilele cha vita dhidi ya Iran, ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo, Sheikh Mohammed bin Zayed.
🔹 Wakati huohuo, jarida la Marekani la Wall Street Journal limeripoti, likinukuu vyanzo vya ndani, kwamba mkuu wa shirika la ujasusi la Israel (Mossad), David Barnea, pia alifanya ziara za siri nchini UAE angalau mara mbili wakati wa vita hivyo.
🔹 Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ziara za Barnea zililenga kuratibu operesheni zinazohusiana na Iran, zikiwemo kubadilishana taarifa za kijasusi na kupanga mashambulizi.
🔹 Jarida hilo lilidai pia kuwa nafasi ya Abu Dhabi katika vita hivyo haikuishia kwenye ushirikiano wa kiintelijensia pekee, bali UAE ilihusika kwa siri katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran.
🔹 Ripoti hiyo imeeleza kuwa UAE ndiyo nchi pekee, nje ya Marekani na Israel, inayodaiwa kushiriki moja kwa moja katika mashambulizi dhidi ya Iran katika kipindi hicho.