Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al‑Anbiya ametangaza kuwa jeshi la Marekani limetekeleza mashambulizi dhidi ya meli za Iran na maeneo ya pwani, kitendo ambacho kimetajwa kuwa uvunjaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa ikisafiri kutoka eneo la Jask kuelekea Mlango wa Hormuz, pamoja na meli nyingine iliyokuwa ikiingia katika mlango huo karibu na Bandari ya Fujairah, zilishambuliwa na vikosi vya Marekani.

Wakati huohuo, mashambulizi ya anga yaliripotiwa kufanyika kwenye maeneo ya raia katika Bandari ya Khamir, Sirik na Kisiwa cha Qeshm, kwa ushirikiano na baadhi ya nchi za eneo hilo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vilijibu mara moja kwa kushambulia manowari na vyombo vingine vya kijeshi vya Marekani mashariki mwa Mlango wa Hormuz na kusini mwaBandari ya Chabahar, na kusababisha uharibifu uliotajwa kuwa mkubwa.Msemaji huyo amesisitiza kuwa Iran itatoa jibu kali kwa hatua yoyote inayotafsiriwa kuwa uvamizi au uchokozi dhidi ya eneo lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *