Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia zimetangaza kuwa ziko tayari kuondoa baadhi ya vikwazo vinavyohusiana na Iran iwapo Tehran itachukua hatua zilizo wazi na zinazoweza kuthibitishwa kuhusu mpango wake wa nyuklia. Hayo yameelezwa katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo nne.
Katika taarifa hiyo, mataifa hayo yamesisitiza kuwa Iran haipaswi kamwe kupata silaha za nyuklia. Pia yameeleza utayari wao wa kushirikiana na Marekani, Iran pamoja na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ili kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.