Uingereza imetangaza kupeleka ndege za kivita za Typhoon kusaidia kulinda miji na miundombinu muhimu ya Saudi Arabia dhidi ya makombora na droni kutoka Yemen.
Kwa mujibu wa Clash Report, uamuzi huo ulitangazwa Oktoba 20 baada ya ombi la Riyadh.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema ndege hizo zitafanya operesheni za ulinzi wa anga na hazitashambulia vikosi vya Ansarullah nchini Yemen.
Mpango huo unapanua msaada uliotangazwa Septemba, ambao tayari ulihusisha ndege ya Voyager ya kujaza mafuta angani.
Uingereza itapeleka pia ndege ya usafirishaji ya Atlas A400M pamoja na washauri wa kijeshi.
London imetaja kulinda anga, miji na miundombinu ya Saudi kuwa lengo la msaada huo.
Hatua hiyo inakuja wakati mashambulizi ya Saudi dhidi ya Yemen yakiendelea, huku vikosi vya Sana’a vikisema mashambulizi yake dhidi ya vituo vya Saudi ni majibu kwa operesheni zinazolenga Yemen.

Maoni