Mkuu wa zamani wa Jeshi la Israel, Herzi Halevi, amesema baadhi ya mateka wa Israel waliokuwa wakishikiliwa Gaza waliuawa kutokana na mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo.
Halevi ametoa kauli hiyo katika mkutano mjini New York ulioandaliwa na shirika la kisheria la Shurat Hadin, kwa mujibu wa taarifa iliyonukuliwa na The Cradle.
Amesema baadhi ya mashambulizi yalifanyika bila jeshi kujua kuwa mateka walikuwa katika maeneo yaliyolengwa.
Kauli hiyo imeibua tena mjadala kuhusu athari za operesheni za kijeshi za Israel kwa watu waliokuwa wakishikiliwa katika Ukanda wa Gaza.
Halevi pia amepinga madai kwamba shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023, lilitokana na usaliti wa ndani ya jeshi la Israel, akisema hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

Maoni