Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yameathiri takribani asilimia 22.5 ya ardhi ya kilimo, huku wakulima wengi wakikabiliwa na hasara kutokana na uharibifu wa mashamba na miundombinu.
Waziri wa Kilimo wa Lebanon, Nizar Hani, amesema hekta 56,000 za ardhi ya kilimo zimeathiriwa, hasa katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo.
Amesema hekta 52,000 ziko katika majimbo ya Kusini na Nabatieh, huku hekta nyingine 4,000 zikiwa Baalbek-Hermel.
Athari za vita zimeenea pia katika ufugaji, ambapo waziri amesema maeneo ya kusini yamepoteza sehemu kubwa ya mifugo yake.
Uharibifu wa mashamba, mifugo na miundombinu ya kilimo unaongeza changamoto za uzalishaji wa chakula na maisha ya familia zinazotegemea sekta hiyo.

Maoni