Jtt, 2 Novemba 2026

Utaridi CI Media

Habari Ndani ya Sayari.

Iran yataka Lebanon ijumuishwe katika makubaliano ya kumaliza vita

Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York

Iran imesema makubaliano yoyote ya mwisho ya kumaliza vita yanapaswa kuijumuisha Lebanon, ikisisitiza kuwa migogoro ya eneo hilo imeungana.

Hayo ni kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh katika mahojiano yake na shirika la habari la Al Mayadeen baada ya ziara yake nchini Lebanon.

Khatibzadeh alisema Tehran haitazami kumalizika kwa vita dhidi ya Iran kama jambo linaloweza kutenganishwa na mashambulizi yanayoendelea Lebanon.

Alisema amefanya mazungumzo na viongozi wa Lebanon, wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Spika wa Bunge Nabih Berri, katika juhudi za kuoanisha mitazamo ya Tehran na Beirut.

Khatibzadeh aliituhumu Marekani kwa kutotekeleza ahadi zilizomo katika makubaliano ya Islamabad, jambo lililopelekea kuvunjika kwa makubaliano hayo.

Kwa mujibu wake, juhudi za kufikia suluhisho zinapaswa kuhusisha kusitishwa kwa vita katika maeneo yote yanayohusika, badala ya kufunga upande mmoja wa mgogoro huku mapigano yakiendelea katika upande mwingine.

Maoni

Maoni