Alh, 22 Oktoba 2026

Utaridi CI Media

Habari Ndani ya Sayari.

Mjumbe wa Marekani: Kuishambulia Yemen Hakuzai Matunda

Wanajeshi katika mazoezi ya kijeshi Saudi Arabia

Matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya Yemen hayajatoa matokeo chanya yaliyotarajiwa na badala yake yamegonga ukuta, kwa mujibu wa Mjumbe maalum wa Marekani, Tom Barrack, kama ilivyoripotiwa na mtandao wa The Cradle.

Katika tathmini yake, Barrack alibainisha wazi kuwa mkakati huo wa kijeshi umeiacha Saudi Arabia katika hali ngumu kiusalama na kisiasa.

Kauli hiyo nzito inatilia shaka kubwa uwezo na ufanisi wa mashambulizi ya kijeshi kama suluhu ya kufikia malengo yaliyokusudiwa na utawala wa Riyadh.

Hata hivyo, inafaa kusisitiza kuwa tathmini hii ya wazi kutoka kwa Barrack haikuwa tangazo rasmi la kusitishwa kwa mashambulizi ya kijeshi, wala haikuwa mwelekeo wa kufikiwa kwa makubaliano mapya ya kidiplomasia ya kumaliza vita hivyo.

Maoni

Maoni