Afisa wa zamani wa usalama wa Netanyahu akamatwa kwa tuhuma za kumshawishi mtoto

Mamlaka nchini Marekani zimemtangaza kukamatwa kwa Matthew Mahl, aliyewahi kuwa mkuu wa usalama wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na pia luteni katika Idara ya Polisi ya Metropolitan ya Washington, kwa tuhuma za kumshawishi mtoto na kujaribu kupata ponografia ya watoto.

Kwa mujibu wa nyaraka za uchunguzi, Mahl mwenye umri wa miaka 47 alikamatwa katika jimbo la Maryland kufuatia operesheni ya siri iliyofanywa na Ofisi ya Sheriff ya Kaunti ya Harford. Katika operesheni hiyo, afisa wa upelelezi alijifanya mvulana wa miaka 15 na kuwasiliana na mshukiwa kupitia Reddit pamoja na ujumbe wa maandishi.

Ripoti zinaeleza kuwa mawasiliano hayo yaliendelea kwa takribani mwezi mmoja, ambapo Mahl alituma maudhui ya kingono licha ya kuamini kuwa alikuwa akizungumza na mtoto aliye chini ya umri.

Maafisa wanasema mshukiwa alikamatwa mara tu alipofika katika eneo walilokubaliana kukutana na mvulana huyo kwa lengo la kufanya vitendo vya kingono.

Uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *