Washington, DC — Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza tena muda mpya wa kumalizika kwa vita dhidi ya Iran, akisema kuwa mapigano hayo huenda yakachukua “wiki mbili hadi tatu zaidi”.
Hii si mara ya kwanza kwa rais huyo kubadilisha makadirio yake kuhusu muda wa vita. Mwanzoni mwa mapigano, Trump alikuwa ametaja kuwa vita vinaweza kudumu “wiki nne au tano”.
Hata hivyo, wiki mbili baadaye, katika mkutano na waandishi wa habari, alisema: “Tutajiondoa hivi karibuni sana. Labda ndani ya wiki mbili, wiki mbili, labda wiki tatu.”Aidha, tarehe 12 Farvardin, katika hotuba yake katika Ikulu ya White House, Trump alitabiri kuwa vita vitaisha “ndani ya siku tatu zijazo”.
Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wameeleza kuwa kauli zinazotofautiana za rais huyo zimeibua maswali kuhusu mkakati wa Marekani.
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa moja ya sababu za ujumbe unaokinzana wa Trump kuhusu Iran ni kwamba “makadirio yake kuhusu Iran yaligeuka kuwa ya makosa.”Maendeleo zaidi yanatarajiwa huku hali ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu.w