Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Seyed Abbas Araghchi, leo Jumatano amefanya mazungumzo ya simu na Musalia Mudavadi, Mkuu wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu hali ya usalama katika eneo la Asia Magharibi na athari za vitendo vya uchokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kwa usalama wa kikanda.
Pia waligusia madhara ya kiuchumi yanayotokana na hali hiyo kwa maeneo mengine duniani.Waziri Araghchi alieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya ukosefu wa usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Mlango wa Hormuz, akisema kuwa imesababishwa na uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
Alisisitiza umuhimu wa hatua madhubuti za kimataifa kwa ajili ya kulinda Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuwawajibisha wahusika kwa ukiukaji wa sheria na uhalifu unaodaiwa kufanywa.
AKwa upande wake, Waziri Mudavadi alisisitiza umuhimu wa kuheshimu uhuru wa kitaifa na uadilifu wa mipaka ya nchi, pamoja na kuepuka matumizi ya nguvu. Aidha, alieleza kuwa diplomasia ni nyenzo muhimu katika kuleta na kudumisha amani katika eneo hilo.