Viwanda vikubwa vya kusafisha mafuta nchini Israel (Bazan) vimepata pigo zito kufuatia mashambulizi ya makombora kutoka Iran, huku ripoti mpya ikifichua kuwa matengenezo hayo yatachukua hadi mwaka 2028 kukamilika.

Licha ya awali Waziri wa Nishati, Eli Cohen, kukanusha kuwepo kwa uharibifu, ripoti ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyonukuliwa na Channel 12, imethibitisha kuwa mifumo muhimu ikiwemo injini za gesi (turbines), boila za mvuke, na vyumba vya umeme vimeharibiwa vibaya katika Ghuba ya Haifa.

Uharibifu huo unatokana na makombora ya Iran yaliyopenya mfumo wa ulinzi wa “Iron Dome,” na kusababisha hasara inayokadiriwa kufikia dola milioni 200. Hatua hii inatajwa kuathiri vibaya usalama wa nishati nchini humo, huku kukiwa na malalamiko ya udhibiti mkali wa habari kuficha kiwango halisi cha hasara za kivita.

Leave a Reply