Ukraine imeendeleza mashambulizi dhidi ya viwanda vya kusafisha mafuta nchini Urusi licha ya Rais wa Marekani Donald Trump kutaka kusitishwa kwa mashambulizi ya miundombinu ya nishati.
Rais Volodymyr Zelensky alisema katika mahojiano na Financial Times kuwa Ukraine haitofuata masharti hayo.
Baadaye, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema kulikuwa na jaribio kubwa la kushambulia kiwanda cha mafuta katika eneo la Ryazan. Gavana Pavel Malkov aliripoti moto kiwandani pamoja na mashambulizi dhidi ya eneo jingine la viwanda, bila kutaja majeruhi.
Zelensky ameilaumu Urusi kwa kuendelea kushambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine licha ya kauli ya Trump kuhusu kusitisha mashambulizi hayo.
Kwa upande wake, Trump anasema mashambulizi dhidi ya viwanda vya mafuta vya Urusi yanaongeza bei za nishati duniani, hasa dizeli.
Mvutano huo umeweka wazi tofauti kati ya Washington na Kyiv kuhusu namna ya kuendeleza vita wakati gharama za mafuta zikiendelea kuwa suala kubwa la kisiasa.

Maoni