Uchambuzi uliochapishwa na The Cradle umeituhumu Saudi Arabia kwa kutumia tofauti za kimadhehebu kuhamasisha vikosi vinavyopigana dhidi ya Ansarallah nchini Yemen.
Mwandishi Mawadda Iskandar ananukuu vyanzo vya eneo hilo vinavyodai kuwa hotuba za kidini katika misikiti na vituo vya elimu zimekuwa zikitumiwa kuhamasisha mapigano, hasa Taiz na maeneo ya kusini.
Makala hiyo pia inaeleza kuhusu matangazo ya kuandikisha wapiganaji katika eneo la Lahj, ambayo inasema yalitumia lugha ya kimadhehebu dhidi ya Ansarallah.
Kwa mujibu wa uchambuzi huo, juhudi hizo zinafanyika wakati vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia vinakabiliwa na shinikizo la kijeshi kutoka kwa vikosi vya Sana’a.
Hata hivyo, makala inaonyesha kuwa viongozi wa Kisalafi hawana msimamo mmoja. Baadhi yao wameunga mkono makubaliano ya kuishi pamoja na kupunguza mapigano.
Saudi Arabia imetumia mimbari ya Ijumaa katika msikiti wa Makkah wiki hii kushambulia Serikali ya Ansarullah, jambo lililokemewa na viongozi wa kidini.

Maoni