Saudi Arabia imeanza utekelezaji kwa vitendo ushirikiano wake wa ulinzi na Uturuki na Pakistan, huku vita dhidi ya Yemen vikiwa jaribio la kwanza la namna mkataba huo utakavyofanya kazi.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa The Cradle, Kamati ya Kimkakati ya Siasa na Ulinzi ya mkataba huo ilikutana Riyadh Oktoba 5 na kuamua kuanza utekelezaji wa ahadi za ulinzi wa pamoja.
Mwandishi Malek al-Khoury anaeleza kuwa hatua hiyo inaongeza chaguo za usalama za Riyadh na kuathiri mipango ya Israel ya kujenga ushirikiano mpana wa kikanda kupitia makubaliano ya Abraham.
Hata hivyo, washirika hao wana vipaumbele tofauti. Uturuki inaangazia Syria na mashariki mwa Mediterania, Pakistan ina wasiwasi kuhusu India; na hivi karibuni imekuwa na migogoro inayozuka mara kwa mara kati yake na Afghanistan, huku Saudi Arabia ikilenga kulinda miundombinu na mpaka wake wa kusini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amesema Ankara inazingatia kuisaidia Saudi Arabia, lakini imeondoa uwezekano wa kutuma wanajeshi kushambulia Yemen.
Uchambuzi huo unaonyesha kuwa ukubwa wa ahadi za mkataba utategemea maamuzi halisi ya kila mshirika.

Maoni