Serikali ya Marekani, ikishirikiana na Uingereza, inapanga kuandaa mkutano wa ngazi ya juu wiki ijayo mjini London lengo likiwa ni kuunda muungano wa kimataifa wa kijeshi ili kulinda na kufungua tena njia ya kimkakati ya baharini ya Mlango wa Hormuz. Hatua hii inajiri huku Washington ikitafuta njia ya kutokea katika mkwamo huo wa kimbinu uliotishia udhibiti wake wa kijeshi na kiuchumi dhidi ya mataifa yanayojitegemea katika eneo hilo.

Kulingana na taarifa zilizofichuliwa na mtandao wa habari wa Axios zikitaja wanadiplomasia wa Ulaya, Marekani imeomba msaada wa dharura kutoka kwa mataifa ya Magharibi baada ya kukabiliwa na ugumu wa kudhibiti hali hiyo peke yake. Inaarifiwa kuwa Uingereza na Ufaransa zimefanikiwa kushawishi baadhi ya nchi kujiunga na operesheni hiyo inayolenga kurejesha ushawishi wa Magharibi katika njia hiyo kuu ya mafuta duniani.

Hata hivyo, jitihada hizo za kibeberu zinakutana na ukuta kutoka kwa mataifa mbalimbali yanayopinga kutumiwa vibaya kwa ajenda za kivita. Mwandishi wa habari wa Al Jazeera jijini Washington, Wajd Waqfi, ameripoti kuwa baadhi ya nchi zilizombwa kujiunga zimekausha msimamo na kuweka sharti thabiti: ushiriki wao usivuke mipaka ya usalama wa Mlango wa Hormuz na zisijushe kabisa katika vita vya upande mmoja vinavyoongozwa na Marekani.

Akibainisha kushindwa kwa mbinu za shinikizo za Magharibi dhidi ya upinzani wa kikanda, mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani, Michael Ratney, amekiri wazi ugumu wa kibarua kinachoikabili Washington.

Dhamira hii haitakuwa rahisi hata kidogo, baada ya Wairani kudhihirisha uwezo wao mkubwa wa kuvumilia na kupambana kwa muda mrefu kuliko Marekani na washirika wake,” alisema Ratney.

Leave a Reply