Serikali ya Afrika Kusini inaachia takriban hekta milioni 2.5 za ardhi inayomilikiwa na dola kwa wakulima weusi, pamoja na kuwapatia hati za umiliki ili kuongeza ushiriki wao katika kilimo cha biashara.
Rais Cyril Ramaphosa amesema upatikanaji wa ardhi unapaswa kuambatana na fedha, mafunzo, ushauri na teknolojia ili wakulima waweze kuendesha shughuli zenye mafanikio.
Kwa mujibu wa taarifa ya RT, Ramaphosa amesema wakulima weusi wanachangia takriban asilimia 10 pekee ya uzalishaji wa kilimo cha biashara nchini humo.
Ameeleza kuwa ukosefu wa mikopo ya kununua pembejeo, kujenga miundombinu na kuongeza ardhi huwafanya wakulima wengi wapya kubaki katika kilimo cha kujikimu.
Ramaphosa ametaja shamba la maziwa la Redlands, katika jimbo la Eastern Cape, kuwa mfano wa namna msaada wa kifedha unavyoweza kupanua uzalishaji.
Ametoa wito kwa wakopeshaji na kampuni za kilimo kushiriki katika kuwasaidia wakulima, akisema mabadiliko ya sekta hiyo yanaweza kuimarisha uchumi wa vijijini, ajira na usalama wa chakula.

Maoni