Walowezi wa Israel wameshambulia ujumbe wa wanadiplomasia wa Ulaya uliokuwa ukitembelea kijiji cha wakristo cha Taybeh, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
Tukio hilo lilifanyika Oktoba 17 wakati walowezi wenye nyuso zilizofunikwa walipouzingira ujumbe uliowahusisha wawakilishi kutoka Ufaransa, Ubelgiji na Poland.
Ripoti hiyo, ikinukuu redio ya jeshi la Israel, inasema washambuliaji walidai vitambulisho na kuvunja dirisha la gari la ubalozi mdogo wa Ubelgiji.
Bernard Baudoux, meya wa mji wa Aulnoye-Aymeries nchini Ufaransa, alitajwa kuwa miongoni mwa waliojeruhiwa.
Mwanaharakati Amit Orfali, aliyekuwa pamoja na ujumbe huo, alisema washambuliaji walikuwa na marungu na walitoa vitisho vya kuwaua.
Tukio hilo limeripotiwa wakati wa kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya Wapalestina wanaovuna zeituni. The Cradle pia imetaja matukio mengine ya kushambuliwa kwa wakulima na kuharibiwa au kuchukuliwa kwa mazao katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi.

Maoni